
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemteua Mtanzania, Bi. Joyce Msuya kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa misaada ya dharura.
.
Kabla ya uteuzi Bi. Msuya alikuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira wa Umoja wa Mataifa.