
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewahimiza wafugaji kuwa na maeneo ya kulishia mifugo yao ili litawapunguzia migogoro inayowakumba kila kukicha. Waziri Ndaki ametoa wito huo alipokuwa akiongea na wafugaji wa vijiji vya Luhembela na Masumbwe vilivyopo wilayani Mbogwe, mkoani Geita.
