Back to top

Silinde:Sijaridhishwa na kasi ujenzi wa madarasa.

17 December 2021
Share

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa katika mkoa wa Iringa ma kuwataka waongeze kasi ya kuharakisha ukamilishwaji wa vyumba hivyo huku wakizingatia ubora wa majengo na thamani halisi ya fedha ionekane.

Hayo ameyasema baada ya kutembea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmshauri Tano (Kilolo, Manispaa ya Iringa, iringa vijijini, Mufindi na Mafinga) na kukuta ni halmashauri mbili za Mufindi na Mafinga zilizokamilisha ujenzi katika ubora wa hali ya juu kwa vyumba vyote zaidi ya 80 walivyopewa na kukabidhi mkoani kwa ajili ya kupokea wanafunzi wapya.

Aidha Naibu Waziri Silinde amemuagiza Afisa Elimu mkoa wa Iringa Joyce Baravuga kuongeza ufuatiliaji katika sehemu zote ambazo bado wapo nyuma katika ujenzi kwani siku walizoongezewa zimebaki chache na ikiwezekana wafanye kazi usiku na mchana waweze kukamilisha lakini wazingatie ubora .