Back to top

Kaburi lafukuliwa baada ya aliyezikwa kuonekana.

17 December 2021
Share

Jeshi la Polisi mkoani Geita limelazimika kufukua kaburi la mtoto aliyefariki dunia katika Hospitali ya wilaya ya Geita kwa ugonjwa upungufu wa damu mwaka 2017 baada ya mtoto huyo kupatikana Kahama mkoani Shinyanga  hivi karibuni akiwa hai huku akiwa amekatwa ulimi wake na hivyo kushindwa kuzungumza.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita Henry Mwaibambe amewaomba madaktari bingwa Hospitali za Muhimbili, Bugando na KCMC kumsaidia mtoto huyo matibabu ili aweze kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Katika zoezi hilo la kufukua kaburi yamepatikana mabaki ya fuvu la kichwa na mifupa ambapo jeshi la polisi limekabidhi sampuli hizo kwa Mkemia Mkuu wa serikali ili kupata vipimo vya vinasaba ili kujua undani wa tukio hilo.