
Wizara ya Afya imesema Serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na wadau wake kwa mwaka 2021/22 imetoa Tshs. Bilioni 28,467,204,790 kwa ajili ya utekelezaji wa programu ya ujenzi wa miundombinu ya maji vyoo, na vichomea taka katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya vipatavyo 660.Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima wakati akifunga Mkutano wa mwaka wa Maafisa Afya Mazingira.
