Back to top

Timu 15 kati 16 zakubali kuweka nembo ya GSM.

18 December 2021
Share

Baada Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) kukutana na kujadili kuhusu udhamini wa Ligi Kuu msimu wa 2021/22, Bodi hiyo imesema ilipata nafasi ya kushauriana na viongozi wa Klabu zinazoshiriki Ligi hiyo ambapo Klabu 15 kati ya 16 zimekubali kuendelea kutekeleza matakwa ya mkataba wa GSM Tanzania Limited mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya NBC ikiwemo kuweka nembo ya GSM kwenye bega la kushoto la jezi zinazotumika kwa michezo ya ligi hiyo.