Back to top

Ukatili unarudisha nyuma jitihada za serikali.

21 December 2021
Share

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kumerudisha nyuma jitihada za serikali za uchumi wa juu kwa kuwa jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu madhara yake.

Akifungua Kongamano la Kampeni ya Twende Pamoja Kupinga Ukatili wa Kijinsia, amesema ili kufikia lengo la kuwa na uchumi wa juu, unaotegemea viwanda ni muhimu kuwepo na ustaarabu ikiwemo kuheshimu utu wa mtu.

Amesema hata kama taifa litaendelea kujenga reli, shule, hospitali katika mahali ambapo utu wetu unadhalilishwa na kundi moja dhidi ya kundi linguine, vitu vyote hivyo havitakuwa na maana.

Amesema vitendo vya ukatili vinachangiwa na ukosefu wa elimu katika jamii kuhusu jinsi na jinsia, mila na desturi kandamizi pamoja na umaskini, hivyo kusababisha utumikishwaji wa watoto na kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo.