Back to top

Ujenzi vyuo vya VETA ukamilike ndani ya miezi 6.

23 December 2021
Share

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Kasulu ambapo ameagiza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi 29 unaoendelea katika Wilaya mbalimbali nchini ukamilishwe ndani ya miezi sita ijayo, ili kuwezesha wanafunzi kuanza kusoma baada ya serikali kutoa shilingi bilioni 48.5 kwa ajili ya kazi hiyo.