
Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limewakamata watu wawili wakazi wa mtaa wa Bangwe Manispaa ya Sumbawanga wakiwa na mitambo ya kutengenezea fedha pamoja na fedha za noti bandia kiasi cha shilingi millioni tatu na laki sita huku kati ya hizo noti za elfu kumi zikiwa 420, noti za elfu tano 143 na noti za elfu mbili zikiwa 50.
