
Waziri wa Madini Mh. Dotto Biteko ametoa siku saba kwa wamiliki wa mashamba pamoja na wamiliki wa leseni katika mgodi wa Kinyambwiga ulipo wilayani Bunda mkoani Mara kumaliza mgogoro wao ambao umedumu kwa zaidi ya miezi mitatu, wakigombania mashamba yanayodaiwa kuwa na dhahabu na kusisitiza kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo ataufunga mgodi huo.
