
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ameziagiza Halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha zinaongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani kwa kuainisha vyanzo muhimu vya ukusanyaji ikiwa ni pamoja na kuhakikisha bidhaa zote zinazotoka ndani na nje ya nchi kupitia mipaka ya nchi jirani za Zambia na Congo mapato yake yanakusanywa kwa kiwango kinachotakiwa.
