
Waziri wa Madini Dkt.Dotto Biteko ameutaka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa Geita (GGM) kuanza ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme ili waweze kuunganishwa na gridi ya taifa na kuondokana na matumizi ya nishati ya mafuta inayogharimu fedha nyingi wakati serikali imejenga kituo cha kufua umeme karibu na mgodi huo.
