Back to top

Jafo asitisha uchimbaji wa madini ya Nickel.

31 December 2021
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe.Selemani Jafo amesitisha shughuli za uchimbaji wa madini aina ya Nickel katika eneo la mlima wa Yobo wilayani Chamwino mkoani Dodoma kutokana na uchimbaji huo kutokidhi sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kuwataka wataalamu wajiridhishe kuhusu athari za mazingira katika eneo hilo.