Back to top

MWINYI ASEMA KUFANYA MAZOEZI NI KINGA.

01 January 2022
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kufanya mazoezi ni kinga muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na sababu za mfumo wa maisha ya binadamu uliopo hivi sasa.
.
Rais Mwinyi amesema wataalamu wa Afya wamebainisha kuwa kufanya mazoezi ni jambo la msingi na lenye kusaidia sana katika kukabiliana na mfumo wa maisha uliopo, ambapo watu wengi wamepoteza utamaduni wa kutembea kwa miguu, kula vyakula vya asili, kutokupenda kunywa maji na badala yake kuegemea zaidi katika unywaji wa soda na juisi za viwandani.
.
Ameongeza kuwa hivi sasa wananchi wengi wamejikita katika matumizi ya muda mrefu wa Simu janja, Kompyuta na Televisheni, na kuvuta hewa chafu pamoja na matumizi makubwa ya vipoza joto, mambo ambayo ni vigumu kuyaepuka katika mfumo wa sasa wa maisha.