Back to top

DC atoa maagizo kudhibiti ndoa na mimba za utotoni.

10 November 2022
Share

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko, ameagiza wenyeviti wa vijiji na kata, Sungusungu pamoja na wenyeviti wa CCM, kukagua sherehe zote za harusi na ndoa zinazofungwa wilayani humo, ili kudhibiti ndoa na mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikiathiri maisha ya watoto wakike kwa kukatisha masomo.

DC Mboneko ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi wa madarasa mapya yanayojengwa wilayani humo, kwa fedha  za serikali huku wananchi wakichangia nguvu zao kuchimba mitaro, kuchimba mashimo ya vyoo na kusomba mchanga na mawe wakiwa na lengo moja tu wanafunzi waende shule.

Changamoto ya mimba na ndoa za utotoni katika Wilaya ya Shinyanga, imetajwa kuwa imepungua baada ya wananchi kuchangia nguvu zao kujenga shule mpya za sekondari, baada ya serikali kutoa shilingi bilioni 2.2.