
Shirikisho la Mashirika ya Ndege Afrika (AFRAA) kwa kushirikiana na mashirika mengine ya ndege Barani Afrika likiwemo Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuibana kampuni ya utengenezaji ndege ya Airbus, baada ya ndege zake aina ya #Airbus A220 kushindwa kufanya kazi kutokana na hitilafu ya injini, ambapo kampuni hiyo imeshindwa kuwa na injini za ziada ,hivyo kuwasababishia hasara wateja wake wanaotumia ndege hizo, ikiwemo ATCL.
.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, wakati wa kikao cha nne cha baraza la pili la wafanyakazi wa Shirika hilo kilichofanyika Unguja, ambapo amebainisha kuwa watengenezaji hao wanatakiwa kuilipa ATCL fidia ambayo ipo kwenye mkataba, suala ambalo limechukua muda mrefu na kulifanya shirika hilo kupoteza mapato zaidi.
