
Rais wa Zanzibar, na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, amekabidhiwa mfano wa ramani ya mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi .
Rais Dk.Mwinyi akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Mhe.Omar Said Shaaban, amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa mji huo.
Naye Waziri Shaaban, alisema ujenzi wa mji huo wa kisasa utajumuisha ukumbi mkubwa wa mikutano wa kimataifa, hoteli zenye hadhi ya nyota tano,eneo la kisasa la biashara, Makazi ya kisasa ya wananchi, hospitali ya kisasa pamoja na viwanja vya michezo.
