Back to top

PAPA FRANCIS AMWALIKA VATICAN RAIS SAMIA

21 January 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, amealikwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Jijini Vatican, kwa mazungumzo rasmi ya siku mbili.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.January Makamba, wakati akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es Salaam, ambapo amebainisha kuwa Mhe.Rais anatarajia kufanya ziara hiyo mnamo Februari 11 na 12, na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican. 
.
Katika ziara hiyo Mhe.Makamba amesema, Rais Samia ataambatana na waumini wa kawaida wa Katoliki ambao watapata fursa ya kuonana na Papa huku akiendelea kusisitiza kuwa mwaliko huo ni heshima kubwa kwa Tanzania, kwani ni watu wachache sana hupata fursa hiyo.