Back to top

Andre Gomes afanyiwa upasuaji baada ya kuumizwa vibaya.

04 November 2019
Share

Klabu ya Everton imethibitisha kuwa mchezaji wao Andre Gomes baada ya kuumizwa vibaya Jana akiwa uwanjani dhidi ya Tottenham amefanyiwa upasuaji na umekamilika vizuri.

Mchezaji huyo alichezewa rafu  na Son wa Tottenham Hotspurs iliyomtegua kifundo cha mguu wake katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dimba la Goodson Park.

Klabu ya Everton imethibitisha kuwa Andre Gomes upasuaji wake umekamilika salama.
Atakuwa  nje ya uwanja kwa ajili ya kupata matibabu zaidi hospitalini.

Aidha klabu ya Everton imewashukuru mashabiki waliokuguswa na tukio hilo hasa kwa arafa za pole  kwenye mitandao ya kijamii.