Back to top

Drogba 'atia nia' kuongoza soka Ivory Coast.

03 August 2020
Share

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ametuma rasmi maombi yake ya kukiongoza chama cha soka cha nchi yake Ivory Coast Football Federation (FIF).

Drogba alirejesha fomu za maombi yake jana Jumapili na kulakiwa na maelfu ya mashabiki wake.

Uchaguzi wa FIF unatarajiwa kufanyika baadae mwezi ujao na Drogba ni miongoni mwa wagombea wanne waliojitokeza katika kinyang'anyiro hicho.