
Mchezaji Eden Hazard, baada ya kutimiza jukumu lake ndani ya kikosi hicho kutwaa kombe la Europa League kwa kuifunga Arsenal mabao 4-1, amesema kuwa anataka kwenda Real Madrid.
Hazard alifunga mabao 2 kati ya mabao 4-1 ambayo wameshinda mbele ya Arsenal na kutwaa kombe ikiwa ni mara ya kwanza kutwaa taji hilo mbele ya Meneja wao Maurizio Sarri.
Baada ya mchezo kuisha, Hazard amethibitisha kuiacha klabu hiyo ya darajani na kujiunga na klabu ya Real Madrid msimu ujao kwa dau la Euro milioni 115.
Kiungo wa zamani wa Chelsea Cesc Fabregas amekiambia kituo cha runinga cha BT Sport kuwa: "Hazard akiwa na mpira mguuni unategemea kuna kitu kitatokea na wachezaji wote huwa wanapata nguvu mpya. Siwezi kusema kuwa atakuwa ndiye mchezaji bor zaidi katika historia ya klabu ya Chelsea, lakini ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa zaidi kuwahi kumpata."