Back to top

Jumbe nzito dhidi ya Golikipa na mshambuliaji wa Everton kuchunguzwa.

19 October 2020
Share

Jeshi la Polisi Merseyside limeamua kufanya uchunguzi dhidi ya jumbe za twitter zilizokuwa zikiandikwa dhidi ya golikipa wa klabu ya Everton Jordan Pickford pamoja na mwenzake Richarlison ikiwa ni siku chache baada ya mchezo wa dabi ya Mji huo iliyowakutanisha Everton na Liverpool.

Polisi wamesema watawafikisha mbele ya mahakama wale wote ambao wamehusika na kuwaonya kuwa hawako juu ya sheria.

Utakumbuka golikipa wa klabu ya Everton Pickford alimchezea faulo beki wa klabu ya Liverpool Vigil Van Dijk ambaye kwasasa amefanyiwa upasuaji na huku mshambuliaji wa Everton Richarlison naye akitolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo huo kwa faulo aliyomchezea kiungo wa Liverpool Thiago Alcantara.

Sasa wakati kukiwa na taarifa kuwa  Van Dijk anaweza kuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima kuuguza majeraha yake.  

Golikipa wa klabu ya Everton Pickford amekuwa akishambuliwa katika mtandao wa tweeter.

Sasa polisi wamesema kuwa kwasasa wako katika uchunguzi dhidi ya watu wanaowashambulia wachezaji hao katika mtandao wa twitter.

Polisi wameendelea kusema kuwa lugha inayotumika katika mtandao huo sio nzuri haikubaliki katika jamii na ndio maana wamelichukulia swala hilo kwa umakini wa hali ya juu.