Back to top

Kikosi cha Yanga cha jichimbia Morogoro kujiandaa na msimu mpya.

11 July 2019
Share

Kikosi cha timu ya Yanga kipo mkoani Morogoro tayari kwa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ambapo kimejichimbia kwenye Chuo cha Bibilia maeneo ya Bigwa huku kukiwa na ulinzi mkali.

Kikosi cha Yanga kinajianda kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara katika msimu wa 2019/20 huku kikiwa kimesajili majembe mapya kadhaa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema kikosi hicho kimeweka kambi eneo la Bigwa kutokana na kuona kuna usalama zaidi pamoja na uwepo wa utulivu.

Hata hivyo, chanzo cha ndani kimesema kuwa kambi hiyo imewekewa ulinzi mkali na hakuna anayeruhusiwa kuzungumza na wachezaji au viongozi wa benchi la ufundi kama hatambuliki.