Back to top

Kiungo wa Inter Milan kuwa nje ya uwanja kutokana na Majeraha

07 October 2019
Share

Klabu ya soka ya Inter Milan imethibitisha kuwa kiungo wao Stefano Sensi atakuwa nje ya uwanja kwasababu anamajeraha ya misuli ya mguu wake wa kulia.

Hii ni siku moja baada ya mchezo mkali kati ya Inter Milan na Juventus uliomalizika Jana usiku kwa Inter kupoteza mabao 2-1, huku mchezaji huyo akicheza kwa dakika 34 tu na kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Vecino.

Taarifa ya lini atarejea mchezaji huyo inatarajiwa kutolewa hivi karibuni.

Sensi amefunga magoli 3 na kutoa pasi za mwisho 2 katika mechi 7 katika timu yake ya Inter Milan msimu huu.