Back to top

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta akutwa na virusi vya Corona.

13 March 2020
Share

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta akutwa na virusi vya Corona.

Klabu ya Arsenal imetangaza kukifunga kituo chake cha mazoezi na kocha huyo kutengwa kwa kuamini kuwa huenda kuna idadi kubwa ya watu walikuwa karibu naye kocha huyo ikiwemo wachezaji wa kikosi cha Arsenal, viongozi na baadhi ya wachezaji wadogo wa klabu hiyo, hivyo wote watatengwa kwa kuhisiwa kuambukizwa virusi hivyo.

Katika taarifa ya klabu hiyo imesema kuwa kwa wale ambao watakuwa wanaonekana hawakuwa karibu na Mikel Arteta basi watarudi kuendelea na kazi zao katika siku za usoni.