
Kocha Suleiman Matola ametambulishwa rasmi Kuwa kocha mkuu wa klabu ya Polisi Tanzania kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua nafasi ya kocha Mbwana Makata ambaye aliisaidia Polisi Tanzania kupanda ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2019-20.
Timu ya Polisi itatumia uwanja wa timu ya Ushirika moshi kama uwanja wa nyumbani na ndio makao makuu ya Klabu hiyo.