Back to top

Mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele kafungiwa mechi mbili.

09 October 2019
Share

Rasmi Ousmane Dembélé kafungiwa mechi mbili hivyo kuukosa mchezo dhidi ya Eibar na El Classico dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Barcelona aliondolewa uwanjani kwa kadi nyekundu wakati timu hiyo ikivaana na Sevilla wikiendi iliyopita na sasa atakosa michezo miwili ambapo wa kwanza ni dhidi ya Eibar wakati Barcelona wakiwa ugenini na dhidi ya Real Madrid katika dimba la Nou Camp.