
Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Dkt. Damas Ndumbaro amesema mchezo wa gofu umehidhinishwa rasmi kama sekta ya kuutangaza utalii nchini.
Ameyasema hayo katika kufunga shindano la gofu kwa wanawake katika klabu ya gofu la Gykhana huku akisema kwa kufanya hivyo ni kukuza mchezo huo na kujitangaza kimataifa.
Kwa upande wa Rais wa Chama cha gofu wanawake taifa (TLGU) Sophia Viggo amesema shindano lijalo la (All africa Challenge Toffy) itafanyika kwa mara ya kwanza katika klabu ya Dar es salaam Gykhana.
Katika shindano hilo lililopewa jina (Gykhana Ladies Open 2021) Angel Eaton wa klabu ya Lugalo akiibuka mshindi kwa mikwaju 147 huku mfuasi wake akiwa ni Madina Hussein wa Arusha Gykhana aliyepiga mikwaju 156.