Mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga uliopangwa kuchezwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umeahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine kutokana na uwanja kuharibika kwa mvua.
Hata hivyo uwanja wa Ihefu ambao ulipangwa kama uwanja mbadala umeonekana kutokuwa na usalama wa kutosha.