Back to top

Michuano ya watoto wenye mahitaji maalum yaanza Arusha.

09 July 2018
Share

Michuano ya Mchezo wa soka na Michezo mingine kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu walemavu na yatima yenye lengo la kuibua vipaji kwa watoto hao na kupata fursa ya kutumia mchezo kama ajira yameanza kutimua vummbi kwenye viwanja vya shule ya arusha meru jijini Arusha huku watoto wakionesha uwezo mkubwa katika michezo mbalimbali.
 
Wadau wa soka kutoka taasisi za kidini wanasenma wameanzisha michuano hiyo kwa lengo la kutafuta vipaji kwa watoto hao ambao wanakosa fursa ya kutumia vipaji vyao katika kujikwamua kiuchumi baada ya kusahaulika na jamii zinazowazunguka.

Watoto wanaoshiriki michezo hiyo wanasema wamepata faraja kupta fursa ya kuonesha vipaji vyao kwani wanauwezo mkubwa lakini wamekosa nafasi ya kuonekana.