Back to top

Mjamzito auawa kwa kunyongwa na watu wasiojulikana Geita.

20 March 2020
Share

Watu wasiojulikana wamewaua watu watatu katika maeneo tofauti mkoani Geita kwa  kukatwa mapanga usiku wa manane  akiwemo mama mjamzito Rebecca James mkazi wa kijiji cha Masumbwe wilayani Mbogwe aliyekuwa na ujauzito wa miezi nane akiuawa kwa kunyongwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Lotson anasema jeshi hilo linaendelea na operesheni katika maeneo yote yaliyotokea mauaji hayo ya kinyama ili watuhumiwa wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Kamanda Mponjoli anasema mauaji hayo yanahusishwa na imani za kishirikina na wivu wa mapenzi ambapo mwili mmoja kati ya mitatu ulikatwa kiganja ambapo akiitaka jamii kuachana na  vitendo vya imani za kishirikina.