Back to top

Mshambuliaji Joaquín Sánchez Rodríguez asaini mkataba mpya.

26 December 2019
Share

Mshambuliaji wa klabu ya Real Betis Joaquín Sánchez Rodríguez amesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi ifikapo mwaka 2021.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 38 raia wa Hispania mapema msimu huu alifunga ‘hat trick’ yake ya kwanza yaani magoli matatu katika mechi moja katika historia ya maisha yake ya soka na kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwenye historia ya ligi kuu ya Hispania Laliga kufunga ‘hat trick’.

Lakini bila kuonesha kuchoka mchezaji huyo anaendelea kudhihirisha shauku yake katika soka kwa kuongeza mkataba huo mrefu na klabu ya Real Betis.