Back to top

Mwakinyo aahidi makubwa kwa Watanzania Novemba 13.

15 October 2020
Share

Bondia Tanzania Hassan Mwakinyo amesema  atatumia pambano lake dhidi ya Muargentina Jose Carlos Paz litakalochezwa Novemba 13 kuwaonesha Watanzania kuwa hajaridhika na bado ana safari ndefu ya kufikia kilele cha mafanikio wakati atakapotetea mkanda wake wa WBF na kuwania mkanda mwingine wa I.B.A.

Bondia huyo  ameahidi makubwa  kwa mashabiki wake kwa kucheza mchezo tofauti ambao wengi bado hawajawahi kushuhudia akiucheza.