Back to top

Mwamuzi wa Uingereza ateuliwa kuchezesha UEFA Champions Ligi.

19 October 2020
Share

Michael Oliver ameteuliwa kuchezesha mchezo wa UEFA Champions Ligi utakaowakutanisha Bayern Munich na  Atletico Madrid kesho kutwa Jumatano licha ya kuandamwa kwa maneno kwa kushindwa kuumudu mchezo wa Merseyside Derby ikiwa ni siku chache tu. 

Mwamuzi huyo alikuwa akikosolewa vikali kwa kushindwa kumuadhibu golikipa wa klabu ya Everton  Jordan Pickford kwa faulo aliyomchezea beki wa Liverpool Virgil van Dijk katika eneo la 18 faulo ambayo ilimfanya beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi kuumia goti na kuwa nje ya uwnaja.

Katika mchezo huo Oliver hakutoa penati kwa tukio hilo kwa kuwa Van Dijk alionekana alikuwa ameotea wakati wa tukio lile.