Back to top

SERIKALI YAHIMIZWA KUKUZA VIPAJI KATIKA SOKA

21 November 2018
Share

Wadau wa mchezo wa soka Mkoani Tanga wameishauri serikali kuwekeza katika mchezo huo kwa kuanzisha vituo vya kuibua vipaji kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 ili kuunda kikosi cha timu ya taifa itakayofanya vyema katika michuano mbalimbali kimataifa

Awali akizindua ligi  ya kuibua vipaji katika viwanja vya Amani wilayani  Muheza  Mkoani Tanga , Mbunge wa jimbo la Muheza Adad Rajab amesema wameanza mchakato wa kuibua vipaji katika Wilaya ya Muheza ili watoto watakaochaguliwa na jopo la makocha wataunda timu ambayo itawakilisha Mkoa wa Tanga katika mechi na ligi mbalimbali na hivyo kuwa mfano kwa mikoa mingine nchini.