
Shirikisho la Kandanda la Ujerumani - DFB limepinga tuhuma za ubaguzi katika kisa kinachomhusu Mesut Özil lakini likasema linasikitishwa na uamuzi wa mchezaji huyo nyota mwenye asili ya Uturuki kujiondoa katika timu ya taifa.
Taarifa ya DFB imesema shirikisho hilo halijihusishi kwa vyovyote na ubaguzi dhidi ya wawakilishi wake, wafanyakazi, vilabu na utendakazi wa mamilioni ya wafanyakazi wake wa kujitolea.
Aidha shirikisho hilo limekiri kuwa lilifanya makosa katika namna lilivyolishughulikia suala la picha aliyopiga Özil na Erdogan lakini likasema ilikuwa muhimu kuwa Oezil mwenyewe, kama alivyofanya Ilkay Gueondogan, kutoa majibu kuhusiana na picha hiyo, bila ya kuzingatia matokeo ya Kombe la Dunia nchini Urusi.