Back to top

TFF yamfuta kazi Amunike,kutangaza kocha wa muda kuiongoza Taifa Stars

08 July 2019
Share

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kusitisha mkataba na Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Emmanuel Amunike na kusema kuwa litatoa taarifa ya Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo la soka Tanzania imesema Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019.

Aidha Imeongeza kuwa Mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja.