Back to top

Timu ya taifa ya wanawake ya Beach Volleyball kuelekea Cape Verde leo.

15 June 2019
Share

Timu ya taifa ya wanawake ya Beach Volleyball imeagwa na kukabidhiwa bendera tayari kwa safari ya usiku wa leo kwenda Cape Verde kushiriki michezo ya kwanza ya Afrika ya ufukweni ambayo itafanyika kuanzia Juni 18-23.

Kocha mkuu wa timu hiyo Bw.Alfred Selengia amesema malengo ya ushiriki wao ni kuwania nafasi za juu ili kupata fursa ya kushiriki mashindano ya dunia.