Back to top

Viongozi TFF wakacha kikao cha Mwakyembe kujadili suala la Amunike.

10 July 2019
Share

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesikitishwa na viongozi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Kuwa na viburi baada ya kuingia mitini na kutohudhuria kikao alichoiwaita leo hii kujadiliana kilichotokea Afcon na kufukuzwa kwa kocha wa Taifa Stars Emmanuel Amunike.

Dkt.Mwakyembe amesema kama wamemfukuz kocha Emmanuel Amunike kwa kuiga Misri basi waige vizuri, huku akisema Serikali haipingi maamuzi hayo bali iliwaita leo ili watoe mpango mkakati wa sababu ya kumuondoa kocha ambaye hajalipwa takriban miezi mitatu na tunaelekea wapi.

Taarifa zaidi hapo baadae.