Back to top

Wachezaji 3 wa Ngorongoro heroes wajumuishwa katika kikosi.

25 October 2017
Share

Wachezaji watatu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 24 wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania "TAIFA STARS" kitakachoingia kambini Novemba 5 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya benini utakaochezwa ugenini Novemba 11.

Kocha Mkuu wa Stars Salum Mayanga ametaja kikosi ambacho hakina mabadiliko makubwa tofauti na kikosi kilichocheza mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya malawi na kuisha kwa sare ya bila kufungana lakini safari hii amewajumuisha wachezaji wa Ngorongoro Heroes Abdul Mohammed, Dickson Job na Yohanna Mkomola ambao wataungana na kipa ramadhani kabwili katika kikosi hicho kwa ajili ya kupata uzoefu.