
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, SUSAN MLAWI amewataka wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika Bujumbura nchini Burundi kwenda kufanya vyema.
Akizungumza katika hafla maalum ya kuwaaga na kuwakabidhi bendera, Susan amesema kwamba ana imani kubwa maandalizi yamekuwa mazuri na sasa ni kwenda kupigania heshima ya nchi katika mashindano hayo yanayoanza kutimua vumbi Alhamisi mjini Bujumbura.