Back to top

Watu waliokufa kutokana na ajali ya moto Ugiriki yafikia 50

24 July 2018
Share

Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya moto nchini Ugiriki imefikia 50 huku idadi ya majeruhi ikendelea kuongezeka wakati zoezi la uokoaji na uzimaji moto huo ukiendelea katika msitu ambao ndio chanzo cha moto umeanzia na kusambaa katika makazi ya watu wanaoishi karibu na msitu huo.

Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto, mpaka sasa wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo, huku watu walio karibu na msitu huo wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras ameitisha kikoa cha dharura cha baraza la Mawaziri na amesema watafanya lolote linalowezekana la kibinadamu kuhakikisha wanaokoa maisha ya watu.