Back to top

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aichangia Yanga Mil.10.

15 June 2019
Share

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amevitaka vilabu vya soka nchini kutumia vema fursa ya kuwa na mashabiki wengi katika kuvifanya viweze kujitegemea kiuchumi.

Waziri mkuu ameyasema hayo leo katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam na kuichangia klabu hiyo shilingi Milioni 10.

Naye, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa yanga warudishe hisia na mapenzi kwa timu yao kama ilivyo kwa timu ya Simba, pia wawe na ubunifu wa kutengeneza mfumo mzuri wa mapato.