Back to top

Yanga kuwakosa wachezaji wake 5 kwenye mchezo wa leo na Coastal Union.

19 September 2018
Share

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utawakosa wachezaji watano kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Taifa leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Dismas Ten amewataja wachezaji Juma Makapu, Ramadhan Kabwili, Pius Buswita na Haji Mwinyi wataukosa mchezo huo kwa sababu ya makosa ya kinidhamu.

Ten amesema wachezaji hao waliondolewa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kwa sababu za kinidhamu ambazo zilimkwaza Mkongo huyo na kuamua kuwapa adhabu ya muda .