Back to top

“Tutachukua hatua kwa wamiliki wa migodi wanaohatarisha usalama"Biteko

16 December 2019
Share

Waziri wa madini Mhe.Doto Biteko amewaagiza wamiliki wote wa migodi wa ndani na nje ya nchi kuwasilisha mipango ya ufungaji migodi mara uchimbaji unapoanza ambapo hadi sasa ni wamiliki 10 pekee waliowasilisha mpango huo kati ya wamiliki mia mbili hali inayohatarisha usalama wa mazingira katika migodi hiyo .

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa la wadau wa sekta ya madini ambapo amesema serikali imejiimarisha kuhakikisha kuwa mazingira na jamii inayozunguka maeneo ya migodi hayaathiriki kutokana na shughuli za uchimbaji madini

Kwa upande wake mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idriss Kikula amesema ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini ni muhimu .

Awali akizungumza kuhusu kongamano hilo makamu wa rais wa kampuni ya Geita Gold Mining GGM Bw.Simon Shayo amesema kupitia kongamano hilo litawezesha wadau wa sekta ya madini nchini kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira na kuwasilisha mpango wa ufungaji migodi kwa maslahi ya taifa.