Back to top

”Kama serikali hatutaingilia bei ya mazao”.Bashe.

11 November 2019
Share

Serikali imesema haitoingilia suala la kushusha bei ya mazao ya chakula kwani kwa muda mrefu wakulima nchini wamekuwa wakipata hasara kutokana na kupangiwa bei ya mazao yao.

 Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mh Hussen Bashe wakati akijibu swali la mbunge wa Busega Mhe. Raphael  Chegeni juu ya kupanda kwa bei ya chakula hususani mahindi na kuongeza gharama ya maisha kwa watanzania.

 Amesema katika kupunguza gharama ya bei ya chakula sokoni serikali inajikita katika kupunguza gharama ya uzalishaji na kuruhusu ushindani sokoni lengo ikiwa pia kumsaidia mkulima kupata faida ya mazao yake.

 Aidha amewataka viongozi wakiwemo wa mikoa kuwasiliana na wakala wa chakula nchini wanapoona kuna upungufu wa chakula katika maeneo yao ili kusaidia kusambaza chakula sokoni ambapo pia amewahamasisha wadau na wakulima kuongeza uzalishaji kama njia ya kupambana na upungufu wa chakula katika maeneo.