
Asilimia 50 ya vifo vya kinamama nchini vinatokana na ungonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi pamoja na saratani ya matiti, hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kupima afya zao mara kwa mara ili wakigundulika mapema kuwa na ugonjwa huo waweze kupatiwa matibabu.
Hayo yamebainishwa na Mke wa Rrais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma kikwete, wakati akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Lindi na vitongozi vyake kwenye uzinduzi wa kampeni ya upimimaji wa saratani za matiti na mlango wa kizazi, kifua kikuu na magonjwa yasio ya kuambukiza.
Dk.Marry Charles ni Rais wa chama cha madaktari wanawake Tanzania mewata akazungumzia lengo la kampeni hiyo huku Mganga mkuu wa mkoa wa Lindi akielezea hali ya ugonjwa wa kifua kikuu mkoani humo.