Back to top

Abiria 60 wanusurika kifo baada ya basi la Saratoga kuteketea moto.

20 August 2018
Share

Takribani abiria 60 wamenusurika kufa baada ya Basi la kampuni ya Saratoga linalofanya Safari zake kati ya Kigoma na Sumbawanga kuteketea kwa moto katika eneo la KAZURAMIMBA wilayani uvinza.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kigoma MARTIN OTIENO  amesema mpaka sasa bado chanzo cha moto huo katika basi hilo lenye namba za usajili T 476 ADG  hakijajulikana na wanaendelea kufanya uchunguzi.

Kamanda  OTIENO amesema kuwa kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuokoa Sehemu kubwa ya mizigo ya abiria waliokuwamao katika basi hilo pamoja huku wakiendelea kufatilia thamani ya mizigo iliyotoketea.