Back to top

Abiria zaidi ya 800 wakwama kwa zaidi ya saa 10 baada ya reli kuzibwa.

01 November 2018
Share

Mamia ya abiria wa treni ya reli ya kati kutoka Kigoma kuelekea mikoa ya bara wamekwama mjini Dodoma kwa zaidi ya saa kumi  baada ya reli hiyo kuzibwa na mabehewa ya mizigo yaliyodondoka eneo la Igandu Dodoma.

ITV imefika katika stesheni ya Dodoma na  kuzungumza na abiria hao ambao wamesema wanakutana na changamoto ya huduma duni ya chakula na vyoo katika eneo hilo.