Back to top

ACP Hamduni amekuwa Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana ahamishwa.

24 June 2020
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amefanya uhamisho kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa ili kuongeza ufanisi na tija katika kazi za Polisi. 

Miongoni mwa waliohamishwa, amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana amehamishwa kwenda kuwa Afisa Mnadhimu namba moja katika Shule ya Polisi Moshi.

Pia (IGP) Sirro, amemhamisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Bunge, Dodoma ACP Emmanuel Lukula kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na nafasi yake inachukuliwa na ACP Andrew Satta ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Polisi Dodoma.